Cherop na Sang watwaa dhahabu Trinidad

Dismas Otuke
1 Min Read

Nancy Cherop na Josephat Sang walinyakua dhahabu katika mbio za mita 1500, katika makala ya saba ya Michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Trinidad na Tobago Jumanne usiku.

Nancy Cherop akikamilisha fainali ya mita 1500

Cherop ambaye pia ni bingwa wa Afrika alitwaa ubingwa katika mbio za wanawake kwa dakika 4 sekunde 12 nukta 28,akifuatwa na Mkenya mwenza Janet Chepkoech aliyeshinda medali ya fedha kwa muda wa dakika 4 sekunde 14 nukta 34.

Josephat Sang akikamilisha fainali ya mita 1500

Josephat Sang alintakua dhahabu ya mita 1500 kwa wanaume akitumia dakika 3 sekunde 37 nukta 66 naye Andrew Kiptoo akashinda fedha kwa kutumia muda wa dakika 3 sekunde 38 nukta 12.

Kenya imezoa dhahabu mbili na fedha tatu katika michezo hiyo itakayokamilika Agosti 11.

Fedha nyingine ya Kenya ilinyakuliwa na Titus Maundu katika shindano la urushuji kijishani kitengo cha F42.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *