Chepng’etich ajikaza kisabuni na kuzoa dhahabu ya mita 10,000 Michezo ya Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Janeth Chepng’etich alijizatiti na kunyakua medali ya dhahabu ya mbio za mita 10,000 Alhamisi usiku, katika michezo ya Afrika mjini Accra ,Ghana.

Chepng’eticha aliye na umri wa miaka 25, alikuwa katika kundi la uongozi huku wakibadilishana nafasi ya kwanza mara kadhaa na Waethiopia Belew Kefale,Behre Amare na Ayana Mulia.

Hata hivyo Mkenya huyo alifyatuka na kumwacha Kefale katika mita 50 za mwisho, na kushinda dhahabu ya sita ya kenya akitumia dakika 33 na sekunde 37, wakati Kefale na Amare wakiridhia fedha na shaba mtawalia.

Medali hiyo imeipaisha Kenya hadi nafasi ya 9 katika msimamo kwa dhahabu 6 fedha 6 na shaba 12.

Website |  + posts
Share This Article