Chebet avunja rekodi ya dunia ya Kilomita 5

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 5,000 na 10,000 Beatrice Chebet,  alivunja rekodi ya dunia ya kilomita 5 jana katika mbio za Cursa dels Nassos mjini Bercelona Uhispania.

Chebet aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa dakika 13 sekunde 54,akivunja rekodi ya awali kwa sekunde 19.

Chebet ambaye pia ni bingwa mara mbili wa dunia katika mbio za nyika, pia anashikilia rekodi ya mita 10,000 ya dakika 28 sekunde 54.14.

Medina Eisa kutoka Ethiopia alimaliza wa pili kwa dakika 14 na sekunde 23, huku Belinda Chemutai wa Uganda akichukua nafasi ya tatu kwa dakika 14 na sekunde 36.

Matthew Kipkoech Kipruto wa Kenya aliibuka mshindi wa mbio za wanaume kwa dakika 13 na sekunde 28.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *