Beatrice Chebet aliongoza Kenya kunyakua nishani za dahahbu na fedha katika fainali ya mita 5000 katika siku ya nane ya mashindano ya Riadha Duniani Jumamosi alasiri.
Chebet ambaye pia alikuwa ameshinda dhahabu ya mita 10,000 ,ameziparakasa mbio za mbio za mita 5,000 kwa kutumia muda wa dakika 14:54.36.
Bingwa wa dunia wa mita 1500 Faith Kipyegon ameshinda nishani ya fedha kwa dakika 14:55.07, wakati Nadia Batocletti wa Italia akiridhia sahaba kwa muda wa dakika 14:55.42.
Chebet ndiye Mkenya wa pili tangu Vivian Cheruiyot aliponyakua dhahabu za mita 5000 na 10,000 mwaka 2011 mjini Daegu, Korea.
Aidha Chebet anashikilia rekodi za Dunia za mbio za mita 5,000 na 10,000 na kilomita 5.
Kenya ni ya pili kwenye msimamo wa medali kwa nishani 5 za dhahabu, 2 za fedha na 2 za shaba.