Chama cha UDA chataka Raila Odinga ashtakiwe

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwenyekiti wa UDA Cecily Mbarire. Picha/Hisani

Chama cha United Democratic Alliance, UDA sasa kinamtaka kinara za Azimio Raila Odinga kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, kufuatia ghasia zilizozuka jana wakati wa maandamano ya upinzani.

Akihutubia wanahabari katika makao makuu ya chama hicho, mwenyekiti wa UDA Cecil Mbarire alisema serikali lazima ichukue hatua dhidi ya kinara huyo wa upinzani.

Alidai  maandamano hayo yanalenga kuhujumu uchumi na siyo ya kulalamikia gharama ya juu ya maisha.

Aliongeza kwamba maandamano hayo husababisha hasara ya takriban shilingi bilioni tatu kila yanapofanyika.

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wa,  alisema serikali inapaswa kuhakikisha kuwa Raila Odinga, wafadhili wake na waliohusika na uharibifu wa mali wanakabiliwa kisheria.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei alisema wanakusanya ushahidi kufuatia ghasia hizo ambao utawasilishwa kwa mahakama ya ICC.

Aliongeza kuwa wanapania kuandaa maandamano ya amani nje ya makao ya Raila Odinga na rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Website |  + posts
Share This Article