Chama cha NRM chamuidhinisha Museveni kuwania Urais mwaka 2026

Museveni aliye na umri wa miaka 81 Septemba mwaka huu amekuwa uongozini nchini Uganda tangu mwaka 1986.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama tawala nchini Uganda ,National Resistance Movement(NRM), kimemuidhinisha Rais Yoweri Museveni, kuwania Urais kwa muhula mwingine mwaka ujao.

Hii ina maana kuwa Museveni atakuwa amehudumu ofisini kwa takriban miaka 45.

Museveni aliye na umri wa miaka 81, Septemba mwaka huu amekuwa uongozini nchini Uganda tangu mwaka 1986.

Japo haijatangazwa mpinzani mkuu wa Museveni, katika uchaguzi wa mwaka ujao atakuwa mwanamuziki Robert Kyagulanyi aka Bobby Wine. kwa tiketi ya chama cha  National Unity Platform.

Website |  + posts
Share This Article