Chama cha KUPPET kimesema kitaendelea na mgomo

Tom Mathinji
1 Min Read
Chama cha KUPPET kimesema kitaendelea na mgomo.

Chama cha walimu cha -KUPPET kimesisitiza kuwa kitaendelea na mgomo hadi tume ya kuwaajiri walimu TSC ikubali kuafikia matakwa yao ya kabla ya kurejea kazini.

Chama hicho cha KUPPET kinaitaka tume hiyo ya TSC kushughulikia maswala yaliyoibuliwa na chama hicho.

Akizungumza wakati wa maandamano ya amani eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi, Mwenyekiti wa chama cha KUPPET katika eneo la Kilifi Chiguba Nyale, alisisitiza kuwa chama hicho hakita-yumbishwa na vitisho kutoka kwa TSC,  huku wakishinikiza kuweko masharti na huduma bora za kazi kwa wanachama wao.

Katibu mtendaji wa KUPPET huko Kilifi Caleb Mogere alitoa wito kwa TSC kuajiri kabisa walimu wote 46,000 wa Shule za Junior Secondary badala ya kurefusha kandarasi zao.

Aliikashifu tume ya TSC kwa kusisitiza kuwa walimu wanapaswa kutii agizo la mahakama la kusitisha mgomo huo na ilhali tume hiyo nayo inaendelea kupuuza uamuzi wa mahakama ulioharamisha uanagenzi wa walimu wa Junior Secondary.

TAGGED:
Share This Article