Chama cha Julibee kinachoongozwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, kimeidhinisha ripoti ya maridhiano ya kitaifa.
Mivutano ya mara kwa mara imesababisha chama cha Jubilee kugawanyika katika mirengo miwili, mmoja ukiongozwa na Uhuru huku mwingine ukiongozwa na mbunge mteule Sabina Chege.
Katika taarifa rasmi, mrengo wa Rais Mstaafu ulisema unaunga mkono ripoti hiyo, ukiwa mojawapo wa vyama tanzu katika muungano wa upinzani, Azimio la Umoja.
Haya yanajiri siku moja baada ya muungano wa Azimio la Umoja, kuidhinisha ripoti hiyo kufuatia kikao na wabunge wa cha hicho na kiongozi wake Raila Odinga.
Ripoti hiyo iliandaliwa kwa pamoja na wanasiasa wa serikali na upinzani kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya kuwasilishwa rasmi kwa Rais William Ruto na Raila mwishoni mwa juma lililopita.