Cham ashangazwa na madai ya Semwanga kujisingizia kifo

Alimtaja Ivan kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa ambaye urithi wake bado unaendelea kuishi licha ya kufariki miaka kadhaa iliyopita.

Marion Bosire
1 Min Read

Shakib Cham ambaye ni bondia na mwanabiashara wa Uganda na mume wa Zari Hassan, ameshangazwa na madai kwamba Ivan Semwanga alijisingizia kifo.

Alikuwa akizungumza kwenye mahojiano ambapo alishangaa kilichochochea madai hayo dhidi ya marehemu Ivan aliyekuwa mume wa Zari Hassan.

Shakib alimtaja Ivan kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa ambaye urithi wake bado unaendelea kuishi licha ya kufariki miaka kadhaa iliyopita.

Alisema Ivan alijijengea jina kubwa alipokuwa hai na athari za maisha yake ni miongoni mwa sababu zinazofanya watu waendelee kumzungumzia hata baada ya kifo chake.

Kwa mujibu wa Shakib, kuendelea kuzungumziwa kwa Ivan hakupaswi kutafsiriwa kuwa kuna jambo lisilo la kawaida kuhusu kifo chake, bali ni ishara ya ushawishi mkubwa aliokuwa nao na namna jina lake lilivyoendelea kuwa na nafasi katika jamii.

Aidha, alihoji mawazo yaliyochochea madai kwamba kifo cha Ivan kilikuwa cha kutengenezwa, akisema hakuna sababu ya msingi ambayo ingemfanya mtu kudanganya dunia kuhusu jambo kama hilo.

Kauli za Shakib zinajiri wakati uvumi kuhusu Ivan Semwanga unaendelea kusambaa mitandaoni. Mfanyabiashara huyo alifariki Mei 2017 nchini Afrika Kusini.

Licha ya miaka kadhaa kupita tangu kifo chake, Ivan bado ni mmoja wa watu mashuhuri wanaoendelea kuzungumziwa, huku maisha na urithi wake vikiendelea kuvutia mjadala wa umma.

Share This Article