Mwanamuziki wa Marekani Cardi B anaonekana kukasirishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo ambapo Donald Trump ameibuka mshindi.
Cardi B ambaye alikuwa anamuunga mkono Kamala Harris kwenye kinyang’anyiro hicho alichapisha video ambayo inamyonyesha akiwa kama ambaye ameshtuka na kuandika, “Ninawachukia sana nyote”.
Inaaminika kwamba mwanamuziki huyo aliyehutubia mojawapo ya mikutano ya mwisho ya kampeni ya Harris huko Wisconsin, anaelekeza maneno hayo kwa wote ambao waliamua kumpigia kura Trump.
Katika hotuba yake siku hiyo, Cardi alidhihirisha wazi kwamba haamini Trump atakuwa bora kwa uchumi wa Marekani, akisema kwamba ni kiongozi anayejijali.
Alisema pia kwamba Trump anataka tu kujitajirisha na kupunguzia mabilionea ambao ni marafiki zake ushuru.