Mabingwa mara tano wa kombe la Afrika AFCON, Cameroon ,Algeria na Burkina Faso ndizo timu tatu za kwanza kufuzu kwa makala ya 35 ya kipute hicho.
Indomitable Lions ya Cameroon walijikatia tiketi jana baada ya kuwalaza Harambee Stars ya Kenya bao moja kwa nunge jijini Kampala,Uganda.
Cameroon walioshinda mechi tati na kutoka sare moja wanongoza kundi J kwa pointi 10 sawia na Zimbabwe iliyo ya pili hku Kenya ikiwa ya tatu kwa alama 4.
Dessert Foxes ya Algeria pia ilijikatia tiketi kufuatia ushindi wa goli 1 kwa bila ugenini jana dhidi ya Togo mjini Lome katika kundi E.
Algeria inayojivunia rekodi ya asilimia 100 inaongoza kundi E kwa alama 12, baada ya mechi 4 ,ikifuatwa na Equatorial Guinea kwa pointi 7.
Burkina Faso almaarufu The Stallions iliwacharaza Burundi mabao 2 kwa nila jana kundini L,na kuongoza kwa pointi 10,tatu zaidi ya Simba wa Teranga ,Senegal walio katika nafasi ya pili.
Cemeroon,Algeria na Burkina Faso wanajiunga na wenyeji Morocco kwa makala ya 35 ya AFCON yatakayoandaliwa kati ya Disemba na mwaka ujoa na Januari mwaka 2026.