Cameroon yarejesha mikakati ya kuzuia msambao wa COVID-19

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Cameroon imetangaza kurejesha baadhi ya sheria kali za kuthibiti kuzuka upya na ongezeko la visa vya ugonjwa wa Covid 19, ambavyo vimeripotiwa barani Ulaya,mashariki ya kati na mataifa ya Afrika.

Kulingana na sheria hizo mpya kutoka kwa wizara ya afya wasafiri wote kutoka mataifa ya kigeni ni sharti wajaze fomu za kujitambulisha punde wanapowasili katika viwanja vya ndege.

Pia wasafiri wote wanaowasili ni sharti wafanyiwe vipimo dhidi ya Covid 19 .

Sheria za awali za kuzuia msambao wa Covid 19 kama vile kuvalia barakoa na kwa watu walio na dalili za homa pia zimerejeshwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *