Bwenyenye Hasmukh Kanji Patel mmiliki wa Mombasa Cement afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Bwenyenye anayemiliki kampuni ya Mombasa Cement Hasmukh Kanji ameaga dunia Alhamisi adhuhuri, baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa na umri wa miaka  58.

Kifo cha Patel ambaye amekuwa akiendesha miradi kadhaa ya kuwasaidia wasiojimudu katika jamii katika kaunti za Kilifi,Mombasa na Kwale kimetangazwa na mwakilishi wodi wa eneo la Tudor Samir Bhaloo.

Yamkini marehemu ambaye hadi kifo chake amekuwa afisa Mkuu mtendaji wa Mombasa Cement aliaga dunia mida ya saa saba leo.

Kanji Patel anadaiwa kuhisi maumivu ya tumbo akiwa nyumbani kwake alipofariki .

Kanji amekuwa akiendesha miradi kadhaa ya kusaidia jamii ikiwemo kuwalisha yatima na vijana wa mitaani katika bustani ya Kibarani Miracle, uliokuwa ukiwalisha takriban watoto 40,000 kila siku.

Pia Marehemu alikuwa akitoa msaada wa jeneza kwa familia maskini kutoka kaunti hizo tatu za eneo la pwani.

Miongoni mwa waliomwomboleza Patel ni Gavana wa kaunti ya Mombasaa Abdulswamad Nassir,aliyemtaja kuwa mkarimu na mshirika wa karibu kwa uongozi wa kaunti ya Mombasa.

Website |  + posts
Share This Article