Butere, Musingu, Kimilili, Tigoi wahifadhi ubingwa wa kitaifa.

Boniface Mutotsi
2 Min Read

Shule za Musingu,Tigoi,Butere na Kimili zote za eneo la Magharibi, zimehifadhi ubingwa wa kitaifa wa mashindano ya shule za sekondari katika kaunti ya Mombasa.

Kwenye mchezo wa magongo, Musingu wamewakwatua tena St. Antony goli moja kwa bila katika Mechi ya uhasama na yenye ushindani mkali, ikiwa marudio ya mwaka jana huko Machakos.

Vipusa wa Tigoi wamehifadhi taji hiyo kwa kuwazaba St. Joseph magoli tatu kwa mawili nayo Ngi’ya ikawa ya tatu.

Katika raga ya wachezaji 15 kila upande, wavulana wa Vihiga walitawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza walipowazaba Kisii alama 14 kwa sita.

Mabingwa wa mwaka jana All saints kutoka Embu,walimaliza wa tatu walipowalemea Upper Hill alama 19 kwa tano.

Katika kikapu, Mabingwa mara tisa na washindi wa mwaka wa 2023 mjini Eldoret -Laiser Hill ndio mabingwa wapya kufuatia ushindi wa alama 71 kwa 69 dhidi ya mbingwa wa mwaka jana – Dr. Aggrey.

Upande wa akinadada, Butere waliganda na taji hiyo kwa ushindi wa alama 76 dhidi 51 za Kaya Tiwi. St. Joseph ya Bonde la Ufa waliridhia nafasi ya tatu.

Katika mpira wa mikono ambapo St.Luke’s Kimilili walikatalia taji hilo kwa ushindi wa alama 35 kwa 17 za St.Alberto’ s Kamito, wakati Highway wakimaliza katika nafasi ya tatu.

Warembo wa Moi Girls Kamusinga pia kutoka Magharibi walitetea taji lao dhidi ya St. Joseph, kisha nafasi ya tatu ikawa ya Dagoretti Mixed.

Pia kuliandaliwa riadha mbali mbali na washindi kutuzwa.

Washindi hao watawakilisha taifa katika mashindano ya Afrika mashariki yatakayoandaliwa nchini Kenya Agosti mwaka huku.

Boniface Mutotsi
+ posts
Share This Article