Klabu ya Butali Warriors waliibuka mabingwa wa ligi kuu ya magongo msimu wa mwaka 2023/2024 baada kuzoa alama 43 kufuatia kutok sare ya mabao mawili katika mchuano wa kufunga msimu dhidi ya Western Jaguars.
Western Jaguar waliibuka wa pili kwa alama 41 nao polisi wakamaliza wa tatu.
Hata hivyo Butali hawakutuzwa medali katika hafla iliyoandaliwa kutokana na kesi iliyowasilishwa kotini na Jaguars kupinga alama za bwerere walizopewa KCA dhidi Butali.
Kwenye kitengo cha akina dada, Blazers,Lakers na USIU walitwaa nafasi za ,kwanza, pili na tatu mtawalia huku Maureen Okumu wa Blazers akiibuka mfungaji bora kwa magoli 11, naye Melody Nyagaka wa Kenyatta University akawa mchezaji bora.
Ligi ya daraja ya pili ya wanaume ilishuhudia Dakiyo, Chuo kikuu cha Eldoret na Parkroad Badgers wakinyakuwa nafasi za kwanza,pili na tatu katika usanjari huo.
Sliders, Mombasa Sports Club na Twinkle walimaliza katika nafasi za 1,2 na tatu mtawali huku Charity Majimbo wa Sliders, akitwaa taji la mfungaji bora wa mabao 29 naye Mary Georgin kutoka Klabu ya Michezo ya Mombasa akazawadiwa kama mchezaji bora.
Ligi ya daraja ya tatu ilinyakuliwa na Kitale wakifuatwa na chuokikuu cha Nairobi huku Kiss wakimaliza wa tatu.