Nyota wa mtindo wa Afrobeats wa muziki kutoka Nigeria Burna Boy alipigana na mpiga muziki DJ Tunez, Jumatatu katika kile kilichotajwa kuwa sherehe ya nyumbani jijini Lagos.
Video zilizosambaa mitandaoni zinaonyesha wawili hao wakirushiana mikono na kupigana huku hali ikibadilika na kuwa mbaya pale ambapo walinzi wa Burna Boy wanapoingilia kati.
Burna Boy na wenzake, wanaonekana kumzidi nguvu Dj Tunez ambaye ni mpiga muziki rasmi wa mwanamuziki Wizkid.
DJ Tunez aliangushwa chini kwenye sakafu wakati wa mvutano huo wakati ambapo watu wengine waliokuwepo wanaonekana kujaribu kuingilia kati bila mafanikio.
Vita vilipokwisha, walinzi wa Burna walimeleka kwenye gari lake.
Kulingana na DJ Tunez, Burna Boy ndiye alianzisha vita kwa kumpiga kwanza nyuma kichwa lakini Burna Boy hajazungumza lolote kuhusu tukio hilo.
Badala yake, amechapisha video inayomwonyesha akichezea wimbo wa “Money Constant” ambao umeimbwa na Dj Maphorisa, Dj Tunez, Wizkid na Mavo kitendo ambacho wengi wametafsiri kama kejeli kwao.