Bunge la Taifa kuandaa warsha ya siku tatu mjini Naivasha

Tom Mathinji
1 Min Read
Bunge la Taifa kuandaa warsha ya siku tatu Naivasha.

Bunge la Taifa limeandaa mkutano wa siku tatu mwishoni mwa mwezi huu mjini Naivasha kaunti ya Nakuru, kutathmini utendakazi wa bunge hilo na pia kupanga ratiba ya mwaka 2025.

Wakati wa kikao maalum Alhamisi alasiri, Spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula, alisema mkutano huo utaandaliwa kati ya tarehe 27 hadi 31 Januari, 2025.

“Mkutano huo ambao unajiri katikati ya bunge la 13, utatoa fursa kwa wabunge kupigia darubini hatua zilizopigwa katika awamu za kwanza tatu na kupanga mikakati kuhusu ajenda za awamu ya nne itakayoanza mwezi Februaru,” alisema Wetang’ula.

Kulingana na Spika huyo, mkutano huo utajumuisha vikao vya mijadala pamoja na vikao vitakavyoongozwa na wataalam wakiwemo wabunge wa sasa na wale wa zamani.

Katika mkutano huo, wabunge wanatarajiwa kuimarisha michakato ya kisheria ili kuboresha utoaji huduma.

Bunge la taifa huandaa mikutano ya katikati ya muhula, kupigia kurunzi ufanisi ulioafikiwa katika uratibu wa sheria na kupanga mikakati ya vikao vya vijavyo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *