Bunge la Kitaifa litaandaa kikao maalum Januari 16 kujadili maswala ya dharura ya kitaifa.
Spika wa bunge hilo Moses Wetang’ula amesema alipokea ombi la kiongozi wa walio wengi Kimani Ichung’wah tarehe 3 mwezi huu, kuitisha kikao maaluma cha bunge lote.
Ajenda kuu ya kikao hicho cha Alhamisi wiki ijayo ni pamoja na:- kuwasilisha ujumbe wa dharura kutoka kwa Baraza la Mawaziri, kuwasilisha miswada kuhusu kupigwa msasa kwa mawaziri watatu wapya, kujadili uteuzi wa Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na kuwapiga msasa Mabalozi wateule.
Hoja zingine ni kujadili mswada wa ugavi wa mapato kwa kaunti, kujadili uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Mishahara na Marupurupu, SRC na hoja nyinginezo.
Kikao hicho cha asubuhi kitaandaliwa kuanzia saa nne huku kile cha mchana kikiandaliwa kuanzia saa nane unusu.