Bunge la Afrika Kusini kufunguliwa Julai 18

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza kuwa bunge litafungiliwa upya baada ya uchaguzi mkuu Julai 18 .

Ramaphosa bado hajatangaza baraza la mawaziri tangu ashinde muhula wa pili wa Urais, ingawa alikosa kuafikia wingi wa viti bungeni na kulazimika kubuni serikali ya muungano .

Yamkini kuwa Rais huyo amekabiliwa na vikwazo vingi katika juhudi za kuunda serikali ya muungano, huku chama chake cha African National Congress (ANC) kikikosa kuafikiana na kile cha Democratic Alliance(DA) kuhusu ugavi wa nyadhfa serikalini.

Kumeripotiwa kuwa na sintofahamu ambapo yamkini Ramaphosa amemshutumu kiongozi wa chama cha DA John Steenhuisen,kwa kukiuka mwafaka wa awali wakupewa wizara sita na badala yake kutaka wizara nane.

Ramaphosa na Steenhuisen wamekuwa na vikao vya ana kwa ana kujaribu kutafuta suluhu.

Serikali ya muungano wa kitaifa ya Afrika Kusini inajumuisha vyama vinane vya kisiasa.

ANC ilizoa asilimia 40 ya kura katika uchaguzi mkuu wa Mei 29, huku DA kikipata asilimia 21 na vyama hivyo viwili vilisaini mkataba wa kubuni Muungano Juni 14.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *