Kamati ya bunge kuhusu uteuzi serikalini imetangaza kufawapiga msasa Mawaziri wateule tarehe 14 mwezi ujao katika majengo ya Bunge.
Mawaziri walioteuliwa watakaosailiwa ni kutathmini ufaafu wao bi pamoja na aliyekuwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ambaye ameteuliwa kuwa waziri mpya wa Kilimo,Gavana wa zamani wa Kiambu William Kabogo ambaye ni Waziri mteule wa Teknolojia ya Habari ,Mawasiliano na uchumi Dijitali pamoja na Gavana wa zamani wa Nakuru Lee Kinyanjui ambaye ameteuliwa waziri wa biashara ,uwekezaji na viwanda.
Kagwe ameratibiwa kuwa wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo itakayoongozwa na Spika Moses Wetang’ula saa sita adhuhuri,akifuatwa na Kabogo saa tisa huku Kinyajui akihitimisha saa kumi na moja jioni.