Bunduki 27 zasalimishwa kwa polisi Turkana

Tom Mathinji
1 Min Read
Bunduki 27 zasalimishwa kwa polisi Turkana.

Maafisa wa Huduma ya Taifa ya Polisi katika eneo la Kainuk, kaunti ya Turkana, wamepokea bunduki 27 zilizokuwa zikishikiliwa na wahalifu.

Kupitia kwa taarifa, huduma hiyo imesema kuwa idadi jumla ya bunduki haramu zilizosalimishwa kwa hiari sasa imefika 247.

“Hatua ya kusalimisha bunduki haramu kwa polisi inaashiria ushirikiano mwema kati ya maafisa wa polisi na jamii katika juhudi za kuimarisha usalama na udhabiti,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi kupitia ukurasa wake wa X.

Aidha, Huduma ya Taifa ya Polisi ilisema itaendelea na operesheni hiyo, ambayo inalenga kuimarisha uwepo wa maafisa wa polisi katika eneo hilo, ili kuzuia kuzuka tena kwa magenge ya wahalifu.

Iliwahakikishia wakazi wa eneo hilo usalama wao.

TAGGED:
Share This Article