Britney Spears asajiliwa katika kituo cha kurekebisha tabia

Anaamini kwamba hatua hiyo itarahisisha keshi inayomkabili ya kuendesha gari akiwa mlevi.

Marion Bosire
2 Min Read

Msanii wa muziki nchini Marekani Britney Jean Spears maarufu kama Britney Spears yuko kwenye kituo cha matibabu ya uraibu wa dawa za kulevya.

Taarifa zinaashiria kwamba aliingia huko siku chache zilizopita katika kituo hicho kilichoko nchini Marekani.

Vyanzo vya taarifa za moja kwa moja vinasema watu wake wa karibu walikuwa wakimsihi ajipeleke mwenyewe kwa matibabu na hatimaye alikubali kufanya hivyo kwa hiari kwani anatambua kuwa amefikia mwisho mbaya kabisa.

Britney amekuwa na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya, hasa Adderall na pombe kwa miaka mingi. Wakati wa safari zake nyingi kwenda Mexico, alikuwa akihakikisha ananunua Adderall.

Vyanzo hivyo vya habari vinasema kwamba Britney aliamua kwenda kwa matibabu akiamini kwamba hatua hiyo itarahisisha keshi inayomkabili ya kuendesha gari akiwa mlevi.

Watu wake wa karibu wanasema kwamba anajua kimkakati kwamba hatua hii itaonekana vizuri mbele ya hakimu, kuwa anachukulia jambo hilo kwa uzito.

Britney alikamatwa kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa katika Kaunti ya Ventura, California tarehe 4 Machi, 2026.

Wanawe na watu wengine wamekuwa wakimuunga mkono sana katika uamuzi huu.

Mpango wake wa matibabu hauna muda rasmi, mara nyingi huwa siku 30, lakini kwa Britney anaweza kukaa kwa muda mrefu zaidi ili aweze kupata nafuu ya maana zaidi.

Share This Article