Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Dunia katika mbio za marathon Brigid Kosgei, atawaongoza wenzake katika makala ya mwaka huu ya mbio za Lisbon Half marathon siku ya Jumapili nchini Ureno.
Kosgei aliye na umri wa miaka 30 anapania kutumia shindano hilo kunoa makali ya msimu .
“Nawashukuru waandalizi wa mbio hizi na ni fahari yangu kuwa hapa .Nataka kukimbia Jumapili ili kupima kasi yangu kwa mashindano ya mwezi ujao ya London Marathon.Ikiwa hali ya anga itakuwa shwari nitajaribu kuvunja muda wangu bora wa saa 1 dakika 4 na sekunde 49.” akasema Kosgei
Kosgei atashindana na bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za mita 5,000 na 10,000 Vivian Cheruiyot, huku pia Jacob Kiplimo wa Uganda akitimka mbio za wanaume dhidi ya Wakenya Abraham Kiptum na Edward Zakayo miongoni mwa wengine