Kocha wa timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande Kevin Wambua ametaja kikosi chake huku akimjumuisha Brian Tanga, anayetwaa nafasi ya Chrisant Ojwang anayeuguza majeraha.
Kikosi hicho kitashiriki mashindano ya Hong Kong Sevens baadaye mwezi huu wakijumuishwa kundi moja na Australia,New Zealand an Marekani.
Kenya ilifuzu kwa mashindano hayo baada ya kupandishwa ngazi kutoka daraja ya pili.
Aidha, timu hiyo ilituzwa shilingi milioni 3.4 na kampuni ya Sportpesa kwa ufanisi huo.
Kocha Wambua amesema lengo lake kuu ni kuhakikisha Kenya inafanya vyema katika mikondo hiyo mitatu itakayohakikisha Kenya inafuzu Kwa mashindano ya msururu wa raga Duniani msimu ujao.
Kikosi kamili
• George Ooro
• Kevin Wekesa
• Vincent Onyala
• Denis Abukuse
• Gabriel Ayimba
• John Okoth
• Samuel Asati
• Nygel Amaitsa
• David Nyangige
• Brian Tanga
• Festus Shiasi
• Patrick Odongo
• Floyd Wabwire