Bingwa wa Dunia katika mbio za mita 5,000 kwa wakongwe Francis Kipkoech Bowen, ameishindia Kenya dhahabu ya pili, katika mashindano ya wakongwe yanayoendelea nchini Marekani .
Bowen ameshinda cha M50 kwa kutumia muda wa dakika 8 sekunde 36.23, akinyakua dhahabu na kuvunja rekodi ya dunia.
Gregory Mitchell wa Marekani amenyakua fedha kwa dakika 9 sekunde 7.85, huku Santiago De La Fuente Martin wa Ufaransa akiridhia shaba.
Ibrahim Makonjo Muyah alikuwa ameshinda fedha ya mita kitengo cha M 40 .
Mashindano hayo ya dunia kwa wakongwe yatakamilika tarehe 30 mwezi huu huku Kenya ikiwakilishwa na wanariadha wanane.