Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria wa ndege iliyoanguka nchini Urusi na kuwaua wote 10 waliokuwa ndani.
Inaaminika kuwa alikuwa ndani ya ndege hiyo.
Ripoti zaidi sasa zinaonyesha kuwa miili minane imepatikana katika eneo la ajali, hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Urusi RIA Novosti.
Tunajua nini?
Kiongozi wa mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin aliorodheshwa kama abiria lakini bado hatuwezi kuthibitisha kwa sasa ikiwa alikuwa ndani ya ndege.
Hapo awali, kituo cha Telegram kinachohusishwa na Wagner, Gray Zone kiliripoti kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.
Bosi huyo wa mamluki mwenye umri wa miaka 62 aliongoza uasi tarehe 23-24 Juni, akiwahamisha wanajeshi wake kutoka Ukraine, na kuuteka mji wa kusini mwa Urusi wa Rostov huko Don, na kutishia kuandamana kuelekea Moscow.
Hatua hiyo ilikuja baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya makamanda wa jeshi la Urusi kuhusu mzozo wa Ukraine.
Mgogoro huo ulitatuliwa kwa makubaliano ambayo yaliruhusu wanajeshi wa Wagner kuhamia Belarusi, au kujiunga na jeshi la Urusi.
Prigozhin mwenyewe alikubali kuhamia Belarusi lakini ameweza kusafiri kwa uhuru, akionekana nchini Urusi na pia inasemekana kutembelea Afrika.
Hotuba ya kwanza ya video ya Prigozhin tangu uasi
Jana tulikuwa tukiripoti kwamba mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin alionekana kwenye hotuba yake ya kwanza ya video tangu maasi yake kushindwa nchini Urusi.
Video hiyo iliyodokeza kuwa alikuwa Afrika, iliwekwa kwenye chaneli za Telegram zilizohusishwa na kundi la mamluki la Wagner.
Ilionyesha Prigozhin katikasare za kijeshi , akisema kundi hilo linaifanya Afrika “huru zaidi”.
BBC haijaweza kuthibitisha ni wapi video hiyo ilirekodiwa.
Wagner inaaminika kuwa na maelfu ya wapiganaji katika bara hilo, ambapo ina shughuli za kibiashara zenye faida kubwa.
Picha yaonekana kuonyesha matokeo ya ajali
Tumepokea picha hii hivi punde, kupitia shirika la habari la Reuters, ambalo linaonekana kuonyesha mabaki ya ndege ikiwaka moto katika eneo lililotajwa kama Tver, magharibi mwa Urusi.
BBC bado haijaweza kuthibitisha nyenzo hii.
Tunajua nini kuhusu ndege iliyoanguka?
Uvumi kwenye chaneli za Telegram ulipendekeza kuwa ndege iliyoanguka ilikuwa ya Embraer Legacy yenye nambari ya RA-02795.
Kufuatilia data kwenye FlightRadar24 – tovuti maarufu ya kufuatilia safari za ndege – haionyeshi ilikotoka.
Mapema leo ilionekana karibu na Moscow, ambapo ilipanda hadi mwinuko wa karibu 29,000ft (8,800m) kabla ya data kuonyesha inashuka ghafla, na kuishia kwa 0ft.
Ndege hiyo imesajiliwa kwa Autolex Transport, ambayo serikali ya Marekani imehusisha na Yevgeny Prigozhin.
Rekodi za safari za ndege sasa hazipatikani kwa kiasi kupitia FlightRadar24.
Lakini imefanya safari kadhaa kwenda na kutoka Moscow na St Petersburg katika miezi ya hivi karibuni, na imepigwa picha na vyombo vya habari vya Belarusi, ambako kundi la Wagner sasa linafikiriwa kuwa na makao yake.
Uchambuzi:Prigozhin alikuwa ameitwa ‘mtu aliyekufa akitembea’
“Mtu aliyekufa akitembea” ndivyo waangalizi kadhaa wa Urusi wamekuwa wakimtaja bosi wa mamluki Wagner Yevgeny Prigozhin tangu alipoongoza maandamano yake ya uasi huko Moscow mwishoni mwa Juni.
Mwitikio wa awali wa Rais Putin kwa changamoto hiyo kwa taasisi ya ulinzi ya Urusi ulikuwa mbaya, akiuita usaliti na ‘kuchomwa kisu mgongoni’ katika ujumbe wa video tarehe 24 Juni.
Ukweli kwamba makubaliano yaliunganishwa kwa haraka ambayo yalisababisha Prigozhin kubaki bila kutarajia na baadaye kutokea Belarusi, St Petersburg na wiki hii, mahali fulani barani Afrika, haikumaanisha kuwa yuko salama.
“Kisasi” alisema Mkurugenzi wa CIA William Burns, “ni lishe ambayo Putin anapendeleakuipakua ikiwa baridi” au maneno yanayokaribiana na hayo.
Hakuna kati ya haya, bila shaka, ni uthibitisho kwamba Prigozhin na wasaidizi wake walilengwa kwa makusudi.
Lakini kutokana na mazingira hayo madai yoyote kwamba kifo chake, kama kitathibitishwa, kilikuwa ni ajali kitashuhudia shauku na maswali mengi