Bongo wawili waongezwa katika hifadhi ya Mlima Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Swara wawili aina ya Bongo wameongozwa katika hifadhi ya wanyama wa mlimani, kama njia ya kuongeza idadi yao.

Mpango huo unaendeshwa na Mount Kenya Wildlife Conservancy, inalenga kuongeza idadi ya wanayama hao ambao ilikuwa imesalia na Bongo 100 pekee .

Jumla ya Bongo 10 wameongeza kwenye hifadhi hiyo katika siku za hivi karibuni.

Kulingana na msimamizi wa mpango huo Dkt Robert Aruho, wanyama hao walikuwa maarufu sana katika maeneo ya milimani lakini idadi yao imekuwa ikipungua kila kuchao.

Kwa kawaida Bongo hao huifadhiwa katika hifadhi ya kando na kisha baadaye kuachiliwa katika mbuga hiyo ya mlimani, ili kujilisha na kujisimamia.

Hifadhi hiyo inapanga kuwaachlia Bongo 50 ifikiapo mwaka 2025.

Share This Article