Bodi ya mamlaka ya biashara na uwekezaji Nyandarua yazinduliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Bodi ya kusimamia mamlaka ya biashara, maendeleo na uwekezaji katika kaunti ya Nyandarua imezinduliwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, gavana wa Nyandarua Daktari Moses Kiarie Badilisha aliwataka wanachama wa bodi hiyo kuchukua hatua za haraka kutambua na kukusanya raslimali na na kuangazia uwekezaji utakaofaidi umma.

Mamlaka hiyo ilibuniwa na sheria ya mwaka 2020 ya biashara, maendeleo na uwekezaji ya kaunti ya Nyandarua na ndilo shirika linalojukumiwa kuongoza uwekezaji wa kilaaina wa kaunti hiyo na linatarajiwa kuongoza juhudi za serikali ya kaunti katika kuongeza thamani bidhaa, utayarishaji wa bidhaa, kutangaza fursa za uwekezaji katika kaunti hiyo na kugeuza uwekezaji wa kaunti kuwa kitega uchumi.

Chini ya uenyekiti wa James Muriu, bodi hiyo itahuisha pia hazina ya biashara.

Uapisho wa wanachama wa bodi hiyo uliongozwa na jaji wa mahakama kuu Charles Kariuki na kushuhudiwa na spika wa bunge la kaunti ya Nyandarua Stephen Waiganjo kati ya wengine wengi.

Share This Article