Bodi Mpya ya Mamlaka ya Afya ya Jamii yazinduliwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha leo Jumatatu amezindua Bodi mpya ya Mamlaka ya Afya ya Jamii, SHA. 

Bodi hiyo ya wanachama sita itasimamiwa na Dkt. Timothy Olweny.

Wanachama wengine ni Katibu Harry Kimtai, Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi, COTU Francis Atwoli, Kaimu Mkurugenzi wa Afya Dkt. Patrick Amoth, Francis Atwoli, Dkt. Zakayo Kariuki, na Jecinta Mutegi.

Wote hao watahumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu katika uteuzi uliofanywa na Waziri Nakhumicha kwa mujibu wa Sheria ya Bima ya Afya ya mwaka 2023.

Bodi hiyo imetwika jukumu la kutekeleza sera zote za serikali zinazohusiana na utendakazi wa Bima ya Afya ya Jamii na majukumu husika.

Hii katika juhudi za serikali za kuhakikisha upatikanaji wa afya kwa wote.

Bodi hiyo inazinduliwa wakati ambapo seriikali iko mbioni kutekeleza Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii, SHIF.

SHIF ni hazina mpya ya serikali inayokusudia kuharakisha ukusanyaji wa mapato yatakayosaidia kuhakikisha azima ya utoaji afya kwa wote inafikiwa.

 

Share This Article