Blackface asema Wizkid na Burnaboy waliiba nyimbo zake

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamuziki wa muda mrefu nchini Nigeria Ahmedu Augustine Obiabo anayefahamika sana kama Blackface amesema kwamba wanamuziki Wizkid na Burna Boy waliiba nyimbo zake na kuzitumia kuandaa kazi zao za muziki.

Mwimbaji huyo anasema anatambua kwamba wanamuziki hao wanajitahidi kuinuka lakini hatua huyo inamfanya ahisi kwamba anashindana na nafsi yake katika ulingo wa muziki.

Blackface anasema haitakuwa tatizo kuwapa watu idhini ya kutumia kazi zake.

Alielezea kwamba Wizkid ndiye alitangulia kuiba wazo kutoka kwa kibao ambacho aliimba na Banky W. Blackface ambaye alikuwa katika kundi la muziki la Plantashun Boiz anasema wizi wa mawazo yake kimziki unaashiria kwamba kazi zake zinapeanwa tu bila idhini.

Hata hivyo, mwimbaji huyo anasema yuko tayari kukutana na kufanya mazungumzo na Wizkid na wenzake kwa sababu anafahamu kwamba wanaibuka na huenda akawapa idhini ya kutumia mawazo yake ya kimziki.

Blackface wa umri wa miaka 49 sasa alianza kazi kama mwanamuziki mwaka 1997 na ni mmoja wa wanachama waanzilishi wa kundi la muziki la Plantashun Boiz.

Anasifika sana kwa ujuzi alionao katika uandishi wa nyimbo ambapo ameandikia wasanii wengine tajika nyimbo nchini Nigeria. Alichangia uandishi wa wimbo “African Queen” wa 2Baba wa mwaka 2004 ambao ulipendeka sana.

Blackface alianza kuimba peke yake mwaka 2004 baada ya kundi la Plantashun Boiz kusambaratika. Mwaka huo huo wa 2004 alitoa albamu iitwayo, “Ghetto Child” ambayo alihusisha wasanii kadhaa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *