Bingwa wa Afrika mwaka 2015 wa mita 3,000 kuruka viunzi na maji Clement Kemboi amefariki katika hali ya kutatanisha.
Mwili wa Kemboi ulipatikana ukiwa unaning’inia kwenye kamba iliyofungwa juu ya mti katika shule ya St Patricks Koisungur mjini Iten, huku miguu ikiwa imetafunwa na mbwa.
Polisi wameanzisha uchunguzi huku mwili wake ukipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa kwa upasuaji.
kemboi aliye na umri wa miaka 33 alipata umaarfu baada ya kushinda dhahabu ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya Afrika iliyoandaliwa nchini Congo.