Mwanamuziki na mfanyabiashara wa Tanzania William Nicholaus Lyimo maarufu kama Billnass amemsifia mke wake Nandy ambaye pia ni mwanamuziki, anaposherehekea siku ya kuzaliwa.
Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Billnass alimshukuru Mungu kwa kumpa mwanamle aliye mzuri, mwenye akili, hekima, busara na upendo.
Alimshukuru Nandy kwa kile alichokitaja kuwa kumzalia mtoto mzuri na kwa kutenga muda wa kumlea vizuri.
“Unanipa furaha kila iitwapo leo kwa kunipa faraja, maneno Mazuri na maono. Natamani sana ulimwengu mzima ujue namna ninavyokupenda.” aliandika Billnass.
Alimalizia kwa kusema kwamba yeye sio mnenaji na kwamba yaliyosalia atayaandika kwenye daftari lao la mapenzi.
Nandy alizaliwa Novemba 9, 1992 katika eneo la Mishi nchini Tanzania. Alifunga ndoa na Billnass mwaka 2022 na wamebarikiwa na binti kwa jina Naya.