Bilioni 1.7 zatengwa kulipa wakulima wa miwa

Marion Bosire
1 Min Read

Wakulima wa miwa watafaidika na bajeti ya ziada ya mwaka wa matumizi ya pesa za serikali wa 2023/2024 kupitia mgao wa shilingi bilioni 1.7, pesa ambazo zitatumiwa kufidia wakulima ambao waliwasilisha miwa kwa viwanda vya sukari vya serikali vya Nzoia, Muhoroni, Chemelili, Sony na Miwani.

Mgao huo unafuatia mapendekezo ya kamati ya bunge kuhusu kilimo na mifugo kwenye ripoti ya mpango wa kuimarisha sekta ya sukari.

Katika mkutano uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Daktari John Mutunga wa eneo bunge la Tigania magharibi, wanachama wa kamati hiyo walikutana na waziri wa kilimo na mifugo Mithika Linturi, katibu katika idara ya mimea Daktari Rono na katibu katika idara ya mifugo John Mueke viongozi hao walidurusu bajeti ya ziada ya mwaka 2023/2024.

Akizungumza kwenye mkutano huo, waziri Linturi alisema kwamba walibuni akiba ya kitaifa ya chakula ambapo shilingi bilioni 2 zilitengwa kwa ajili ya kununua mahindi ili kuhakikisha uwepo wa chakula.

Wanakamati hao waliuliza maswali kuhusu uwezekano wa kujirudia kwa majukumu.

Share This Article