Bidco United yaikaanga Bandari Ligi Kuu ya FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Bidco United United imesajili ushindi wa mabao 2 kwa bila katika mojawapo wa mechi mbili za ligi kuu iliyochezwa Jumatatu katika uwanja wa Kasarani Annex.

Bidco United walichukua uongozi wa mchuano huo kunako dakika ya 22 kupitia kwa Shariff Musa naye Thomas Wainaina akatanua uongozi.

Kenya Commercial Bank waliibwaga Muhoroni Youtha goli moja bila jawabu katika uwanja wa Muhoroni, Haniff Wesonga akitikisha nyavu kunako dakika ya 33 akiunganisha pasi ya Herrit Mungai.

Hata hivyo, msimamizi wa mechi aliwapa Muhoroni Youth ushindi baada ya mashabiki kuzua rabsha na kusimamisha mechi.

Posta Rangers wangali kushikilia kukutu jedwali la ligi kwa pointi 16, wakifuatwa na Gor Mahia na Murang’a Seal wenye alama 12 kila moja.

Share This Article