Bi. Rigathi akariri kujitolea kwa serikali kuimarisha hali ya wafungwa

Dismas Otuke & Lydia Mwangi
1 Min Read

Mkewe Naibu Rais Dorcas Rigathi amekariri kujitolea kwa serikali ya Kenya Kwanza kuimarisha hali ya wafungwa katika magereza ya humu nchini.

Kulingana na Naibu Kamishna wa Magereza Florence Omondi, idadi ya wafungwa katika magereza ya humu nchini imeongezeka hadi zaidi ya wafungwa 62,000 na watoto 300 wanaoandamana na kina mama zao, idadi ambayo ina wafungwa 32,700 zaidi ya kiwango kinachohitajika.

Bi. Rigathi alisema haya leo Alhamisi alipozuru gereza la Rumuruti.

Alisisitiza kuwa serikali ina mipango ya kufungua magereza zaidi ili kumudu wafungwa zaidi na kuounguza misongamano.

Kwa upande wake, Gavana Joshua Irungu alisisitiza haja ya kuyafanyia mabadiliko magerereza kote nchini akiahidi kuwa serikali yake itaboresha vifaa vyote magerezani katika kaunti hiyo kwa kujenga wodi zaidi na kuchimba visima.

Dismas Otuke & Lydia Mwangi
+ posts
Share This Article