Mwigizaji wa Marekani Betsy Brandt ameanzisha mchakato wa kumtaliki mume wake wa miaka 25 Grady Olsen, mwaka mmoja tangu wawili hao walipotengana.
Betsy anaendesha mchakato huo yeye mwenyewe mahakamani bila wakili na ametaja sababu za talaka kuwa tofauti ambazo haziwezi kurekebishwa.
Katika stakabadhi za mchakato huo, Brandt anasema kwamba walifunga ndoa Septemba 1998 na walitengana Agosti 2023.
Amefafanua kwamba yeye na Olsen wana mtoto mmoja wa umri wa chini ya miaka 18 na anataka kupatiwa idhini ya kumlea na mahakama.
Kuhusu malimwigizaji huyo ameelezea kwamba itabidi wagawane ikiwa haijulikani iwapo walikuwa na agano la kabla ya ndoa kuhusu mali.
Brandt alipata umaarufu kutokana na uhusika wake kwenye kipindi cha “Breaking Bad” alipoigiza kama ‘Marie Schrader’.
Kipindi hicho kilipofikia mwisho mwaka 2013, Brandt aliingilia kipindi cha vichekesho cha ‘Life in Pieces’ ambapo aliigiza kama ‘Heather Hughes’.