Benni McCarthy kuzinduliwa leo kuwa kocha mpya wa Harambee Stars

Dismas Otuke
3 Min Read

Aliyekuwa mshambulizi wa zamani wa Afrika Kusini Benedict Saul McCarthy, almaarufu Benni McCarthy, anatarajiwa kuzinduliwa leo Jumatatu kuwa mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya, Harambee Stars.

McCathy, ambaye ni mfungaji bora wa Bafanabafana kwa magoli 31, atatwaa ukufunzi wa Kenya kutoka kwa kaimu kocha Francis Kimanzi.

McCarthy, aliye na umri wa miaka 47, anatarajiwa kuandamana na wasaidizi wake akiwemo mkufunzi wa makipa huku pia akitarajiwa kuhudhuria debi ya mashameji kati ya AFC Leopards na Gor Mahia Jumapili hii kuwania alama 3 za Ligi Kuu.

Yamkini McCarthy ataandamana na kipa wa zamani wa timu ya Afrika Kusini na pia kilabu ya Orlando Pirates Moneeb Josephs na Vasili Manousakis watakaokuwa wakufunzi wa walinda lango.

Wasifu wa McCarthy

Alizaliwa: Novemba 12 mwaka 77 (Umri miaka 47) mjini Cape Town

Aliichezea klabu ya Seven Stars mwaka 1996,  kabla ya kujiunga na Capetown kwa mkopo

1998 – Alirejea Sevens Stars mwaka 1998

1997/1998 – Alihama Seven Stars na kujiunga na Ajax Amsterderm ya Uholanzi

1999/2000 – Aligura Ajax na kujiunga na Celta Vigo ya Uhispania

2002 – Alihama Celta  Vigo na kujiunga na FC Porto ya Ureno kwa mkopo

2003 – Alirejea Celta Vigo baada ya kumalizika kwa mkopo wa Porto

2023 – Ajiunga na FC Porto

2006 – Alihamia Blackburn Rovers ya Uingereza kutoka FC Porto

2010 – Ahima Rovers na kujiunga na Westham United ya Uingereza

2011 – Alisalia bila klabu baada ya kutemwa na Westham United

2015 – 2016 – Alikuwa naibu meneja wa klabu ya Sint Truiden ya Ubelgiji

2017-2010 – Meneja wa klabu ya Cape Town  City

2021-2022 – Menaja klabu ya AmaZulu FC

2022-2023 – Kocha wa Washambulizi Manchester United FC

Kibarua cha kwanza kwa kocha huyo mpya ni kuingoza Harambee Stars kwa mechi ya kundi F, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao dhidi ya Gabon mechi ya mwezi huu  jijini Nairobi.

Kenya ni ya nne kundini kwa alama 5, nyuma ya Ivory Coast, Gabon, na Burundi zilizo na alama 10, 9, na 7 mtawalia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *