Benki ya Equity imetangaza faida ya shilingi bilioni 16 ikiwa ongezeko la faida ya shilingi bilioni 12.8, katika robo ya kwanza ya mwaka uliopita.
Afisa Mkuu mtendaji wa benki hiyo James Mwangi amesema faida hiyo ya asiimia 25, kutokana na mikakati bora ya kibiashara .
Hata hivyo faida ya mwaka mzima kutoka kipindi cha Machi 31 mwaka uliopita hadi mwaka huu tarehe 31 mwezi wa tatu mwaka huu, ilipungua kutokana na ulipaji wa mikopo kwa sarafu ya dola ambayo ilikuwa imepanda bei.
Pato la benki hiyo pia liliongezeka kutoka asilimia 21 hadi 28 katika kipindi kicho hicho.
Matawi ya benki hyo katika mataifa ya Uganda,Tanzania,Rwanda ,DRC, na Sudan Kusini pia yalinawiri katika kipindi cha mwaka uliopita.