Maafisa wa polisi wamepata bastola moja ambayo iliibiwa kimabavu kutoka kwa afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Vihiga mwaka jana.
Kulingana na polisi afisa huyo mkuu wa polisi, alishambuliwa na genge la wahalifu Disemba, 31, 2023. Bastola hiyo ilipatikana katika mtaa wa Mwiki, Jijini Nairobi.
Kwenye taarifa katika mtandao wa X, idara ya maafisa wa polisi ww upelelezi wa maswala ya jinai DCI, ilisema jambazi aliyekuwa na bastola hiyo aina ya Jericho, aliuawa kwenye makabiliano baina yake na makachero hao.
Mwili wa mshukiwa huyo umepelekwa katika chumba cha wafu cha City.
Makachero sasa wanawasaka washukiwa wengine wawili waliofaulu kutoweka wakati wa kisa hicho.
Gari la aina ya Nissan Note lenye nambari za usajili za KBZ 985T ambalo majambazi hao walikuwa wakitumia pia lilinaswa kwenye oparesheni hiyo.
Makachero walitekeleza oparesheni hiyo baada ya kupashwa habari za kijasusi kupitia mtandao wa #FichuakwaDCI ..