Basi linalimolikiwa na kampuni ya usafiri ya Tahmeed lilishika moto muda mfupi baada ya abiria kuondolewa karibu na mji wa Voi kwenye barabara kuu ya kutoka Nairobi kuelekea Mombasa.
Lilikuwa na abiria 48 wakati wa kisa hicho cha saa kumi alfajiri kilichohusisha basi lililokuwa likotoka Kitale kuelekea Malindi.
Kulingana na polisi na usimamizi wa kampuni ya Tahmeed, chanzo cha moto huo uliochoma kabisa basi hilo hakijabainika.
Usimamizi huo uliomba radhi abiria kwa hitilafu zilizotokea kwenye safari yao. Wahudumu wa kampuni hiyo waliwasaidia kupata namna ya kukamilisha safari zao.
Hii ni mara ya pili kwa basi la kampuni ya Tahmeed kuchomeka.
Mapema mwaka jana, basi lingine lililokuwa na abiria 42 lilichomeka katika eneo hilo hilo.