Barua za mwito kwa wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu zafutiliwa mbali

Marion Bosire
1 Min Read

Wizara ya elimu nchini imetangaza kufutiliwa mbali kwa barua zilizotolewa na taasisi ya kusajili wanafunzi katika vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu KUCCPS kwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2023 za kujiunga na vyuo vikuu.

Katika taarifa katibu katika wizara ya elimu Beatrice Muganda alisema kwamba barua hizo hazina umuhimu wowote sasa na tangazo lake linalenga wanafunzi wanaokwenda kusomea shahada.

Taarifa ya Muganda inaelezea kwamba kulikuwa na makosa kwenye kiwango cha karo kilichotajwa kwenye barua hizo na akaelekeza kila chuo kikuu kutoa barua mbadala zilizo na kiwango stahiki cha karo kufikia Agosti 5.

Wizara ya elimu hata hivyo imehakikishia wanafunzi hao watarajiwa wa vyuo vikuu kwamba nafasi zao katika vyuo husika na katika kozi walizokuwa wamechagua hazijaathiriwa kwa vyovyote.

Awali kamati ya bunge la taifa kuhusu elimu ilikuwa imeelekeza wizara ya elimu kutupilia mbali barua hizo ambazo wanafunzi walitumiwa kutokana na kiwango cha karo kilichotajwa humo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *