Baraza la Magavana limeishtumu serikali ya taifa kwa kile ilichotaja kuwa juhudi za maksudi za kuangamiza ugatuzi hapa nchini.
Baraza hilo liliangazia suala la kupunguzwa kwa mgao wa wa shilingi bilioni 38.4, fedha ambazo wanadai zimeelekezwa katika serikali kuu.
Akizungumza na wanahabri naibu mwenyekiti wa baraza hilo Mutahi Kahiga hatua hiyo itaathiri utendakazi katika kaunti.
Aidha Kahiga alibainisha kuwa kuna baadhi ya kaunti ambazo hazijapokea fedha tangu mwezi januari mwaka huu, fedha hizo zikifikia malimbikizi ya shilingi bilioni 78.03
Sasa magavana wametishia kusitisha huduma katika kaunti zao iwapo suala hilo halitashughulikiwa.