Barack na Michelle Obama wamwomboleza Rais wa zamani Carter

Wawili hao walichapisha taarifa ya pamoja ambapo walimkumbuka Carter kwa mazuri mbali mbali aliyotenda akiwa hai.

Marion Bosire
1 Min Read
Jimmy Carter, Rais wa 39 wa Marekani

Aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama wamemwomboleza Rais wa 39 wa Marekani Jimmy Carter aliyefariki jana Jumapili.

Obama na Michelle, wanamkumbuka Carter kwa athari zake kwa wamarekani na kwa ulimwengu. Katika taarifa ya pamoja, wawili hao walisifia kujitolea kwa Carter kuhudumia watu na kushikilia maadili mema katika maisha yake.

Walisema kwa miongo kadhaa, Carter angepatikana katika kanisa la Maranatha Baptist huko Plains, Georgia, akitoa mafundisho kwa wageni kutoka sehemu mbali mbali ulimwenguni.

Utetezi wa haki za wanawake ni jambo jingine ambalo Obama na mkewe wanamkumbuka Carter kwalo.

“Alikuwa anaamini kwamba sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na aliishia imani hiyo kwa maadili, heshima na mapenzi” waliandika wanandoa hao.

Baada ya huduma yake kama Rais kufikia mwisho, Carter alihudumia watu kama mhisani ulimwenguni kote ambapo alihusika katika shughuli kama kumaliza ugonjwa wa wadudu nchini Guinea, kusimamia chaguzi zipatazo 100 na kushirikiana na shirika la makazi ya binadamu.

Yeye ndiye rais wa pekee wa zamani kuwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, kutokana na jitihada zake za kuimarisha amani na afya ulimwenguni.

Obama na mkewe walimaliza taarifa yao kwa kutoa rambirambi kwa familia ya Carter na kanisa zima la Maranatha Baptist.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *