Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya (KeNHA) imetangaza kuwa barabara ya Nyerere itafungwa kwa muda karibu na mzunguko wa chuo kikuu cha Nairobi.
Katika taarifa yake, mamlaka hiyo imethibitisha kuwa barabara hiyo itafungwa mnamo Ijumaa, Mei 24, 2024 kuanzia saa tano usiku na kufunguliwa Jumamosi, Mei 25, 2024 usiku wa manane.
KenNHA ilisema itafunga barabara hiyo ili kupisha shughuli za ukarabati wa sehemu hiyo.
Mamlaka hiyo iliwashauri watumiaji wa barabara ya Uhuru (A8) kupitia barabara ya Nyerere, kutumia barabara ya Kenyatta wakipitia Processional Way na Riverside Drive. Pia iliwashauri wapitie State House Road, Arboretum Drive na Ring Road Kileleshwa.
KenHA iliwashauri madereva kukaribia sehemu hiyo kwa tahadhari na kufuata mpango uliopendekezwa wa usimamizi wa trafiki wanaposhirikiana na polisi na wasimamizi wa trafiki kwenye sehemu hiyo.