Barabara ya ndege yafungwa JKIA

Martin Mwanje
1 Min Read

Barabara ya ndege imefungwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA. 

Mamlaka ya Kusimamia Viwanja vya Ndege nchini, KAA inasema hatua hiyo imetokana na kisa kilichohusisha ndege moja, ingawa haikutoa maelezo ya kina kuhusiana na kisa hicho.

“Hakuna majeruhi walioripotiwa. Uondoaji wa ndege hiyo unaendelea,” ilisema KAA katika taaifa kwa abiria.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na tutatoa taarifa zaidi muda mfupi ujao.”

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *