Bangi yenye thamani ya milioni 44 yateketezwa Busia

Saidy Abdallah
1 Min Read
Idara ya usalama mjini Busia imeteketeza bangi yenye thamani ya shilingi milioni 44.1 katika eneo la kutupa taka la Alupe kaunti ndogo ya Teso Kusini.
Kamanda wa polisi wa kaunti ya Busia Mohamed Abdille amesema kuwa bangi hiyo imenaswa wakati tofauti ikiingizwa hapa nchini kutoka taifa jirani la Uganda.
Akizungumza na wanahabari baada ya kunaswa kwa bangi hiyo, kamanda huyo wa polisi amesema kuwa bangi hiyo imekuwa na jumla ya uzani wa kilo 1,400.
Amewapongeza ushirikiano mwema baina ya maafisa wa polisi na wananchi ambao umechangia kunaswa kwa bangi hiyo.
Aidha, msaidizi wa kamishna wa Busia Calvin Munari amesema kuwa visa vya bangi kuingizwa hapa nchini kila mara vimechangia kwa wanafunzi kuathirika kimasomo mbali na wenyeji wanaotumia miahadarati hiyo kujihusisha na uhalifu.
Saidy Abdallah
+ posts
TAGGED:
Share This Article