Bangi ya thamani ya shilingi Milioni 13 yanaswa Busia

Tom Mathinji
1 Min Read

Polisi katika kaunti ya Busia, wanawasaka washukiwa wawili waliotoroka baada ya kufumaniwa na bangi yenye thamani ya shilingi milioni 13 Jumatano.

Maafisa hao walikuwa wakishika doria katika barabara ya Busia Kisumu walipopata bangi hiyo ya uzani wa kilo 451.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), washukiwa hao walitoroka baada ya kuwaona maafisa wa polisi na kuwacha bangi hiyo.

Polisi hao walifanya msako kwenye kichako kilichokuwa karibu na kuona dalili kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wamejificha hapo, hivyo basi kuashiria maficho ya washukiwa hao kabla ya kutoroka.

Bangi hiyo ilisafirishwa kwa gari la polisi hadi kituo cha polisi cha Busia. Polisi wanaendelea na msako wa washukiwa hao.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *