Bandari ya Mombasa haitabinafsishwa, asema Rais Ruto

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto ametoa hakikisho kwamba bandari ya Mombasa haitabinafsishwa. 

Badala yake, Rais Ruto anasema bandari hiyo itapanuliwa ili kuimarisha huduma zake kwa nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja Sudan Kusini na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC.

“Mimi niliwaambia watu wa kutoka Mombasa, mambo ya ubinafsishaji wa bandari ya Mombasa haitafanyika wakati tukiwa serikalini. Niliwaambia kwanza ya kwamba nikifika ofisini, ile maneno ya kuleta CFS Nairobi, ya kuleta operesheni za bandari Nairobi yataisha, tutarudisha operesheni za bandari Mombasa. Na tulifanya hivyo siku yangu ya kwanza ofisini,” alisema Rais Ruto wakati akihutubia Baraza la Kitaifa la Uongozi wa chama cha UDA katika ukumbi wa Bomas leo Ijumaa.

“Ile kitu mimi nataka niwahakikishie ile bandari sasa nataka tuipanue vizuri na tuweke nafasi kubwa zaidi ya kuzalisha ajira na mali kwa sababu ile badari sasa iko na uwezo wa kuhudumia Sudan Kusini, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC, Rwanda, Burundi na majirani zetu wa Uganda.”

Rais Ruto aliahidi kushirikiana na sekta ya kibinafasi kuboresha huduma katika bandari hiyo.

Share This Article