Harakati za klabu ya Bandari FC kutaka kushiriki mashindano ya kuwania kombe la Mapinduzi mwaka huu zimegonga mwamba,baada ya FKF kuwanyima kibali .
Kulingana na FKF Bandari wamenyimwa kibali kutokana na ligi kuu inaoenndelea.
Hata hivyo naibu mwenyekiti wa Bandari Twaha Mbaraka amekanusha madai ya FKF akisema ni mechi moja pekee dhidi Kakamega Homeboyz ambayo ingeathirika endapo wangecheza hadi fainali.
Bandari walipata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo kutoka kwa waandalizi.