Aliyekuwa Waziri wa Utalii Najib Balala,katibu wake wa zamani Leah Adda Gwiyo na afisa wa kampuni ya West Consult Engineers Joseph Odero, wamefikishwa kizimbani Ijumaa adhuhuri katika mahakama ya Malindi kujibu mashtaka ya madaia ya wizi wa shilingi bilioni 8.5.
Watatu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kulipa shilingi bilioni 8.5 kwa ujenzi wa chuo cha Utalii ambacho kwa sasa kinajulikana kama Ronald Ngala Utalii College,eneo la pwani.
Kulingana na EACC Balala alikuwa asafirishwe kwa ndege kutoka Nairobi hadi Mombasa na baadaye kufukishwa katika mahakama ya Malindi.